Ile tabia ya watu maarufu kununua vitu vyenye thamani imeendelea kuongezeka kwa kasi hivi sasa, ambapo Jose chameleone mwanamziki anayetokea UGANDA ametrend kwa kuonyesha viatu vyake viwili vyenye thamani ya dola za kimarekani 12,500. Jose chameleone amesema kununua viatu hivyo hamaanishi kwamba anajionyesha ila ni moja ya njia anayotumia kumshukuru Mungu. Jose Chameleone akiwa amevishika viatu hivyo Jose ni mmoja kati ya wanamuziki wenye mafanikio zaidi kwa wakati huu, ambapo utajiri wake amekuwa akiuweka wazi mara kwa mara kwa kuonyesha magari na nyumba anzozimiliki.
Wapenzi wa bangi na kuabudu wamepata kanisa lao, kanisa hili lipo mjini Denver Marekani na litafunguliwa April 20 ikiwa ni siku ya wavutaji duniani. Taasisi ya dini Elevation Ministries imetangaza uzinduzi wa kanisa hili la kimataifa International Church of Cannabis, ikiwa ni sehemu ya wavutaji kujiskia huru kuabudu.
Waumini wa kanisa hili wanajiita Elevationists, na Jengo la kanisa hili linamiaka 113 na limerekibishwa hivi karibui…
2 Chainz amesha kubali kufanya show kwenye uzinduzi wa kanisa hili.
Forbes imeachia orodha mpya ya wasanii wapaya wanaoingiza mkwanja mrefu zaidi “Forbes Hip-Hop Cash Princes” Kwenye Oorodha hiyo wapo Bryson Tiller ambaye alikuwa akiingiza $100,000 kwa usiku mmoja kwenye tour yake ya muziki huku akiingiza nyimbo mbeli zilioongoza kwenye chart ya Top 40 na album yake ya TrapSoul ikiwa imeenda Platnum,Desiigner mbali ya nomination ya Tuzo za Grammy, Ngoma yake ya Pandaimeongoza chart nyingi ikiwemo Billboard Hot 100 na pia emepata dili nono la kusainiwa kwenye lebel ya Kanye West G.O.OD Music.
Hii ndio orodha kamili, Desiigner D.R.A.M. Tory Lanez Lil Uzi Vert Lil Yachty Noname Isaiah Rashad Stormzy Bryson Tiller Young M.A.
Mwaka jana Boi-1da, DeJ Loaf, Fetty Wap, G-Eazy, Joey Bada$$, Lil Dicky, Logic, na Metro Boomin walitajwa kwenye orodha hiyo.
Forbes wametoa orodha mpya ya waigizaji wa filamu wa kiume wanaolipwa fedha zaidi duniani. Dwayne ‘The Rock’ Johnson ndiye ameongoza orodha hiyo Lakini pia kwenye orodha hiyo kuna waigizaji wa kiwanda cha filamu cha Bollywood,
20. Harrison Ford – $15m 19. Matthew McConaughey – $18m 18. Amitabh Bachchan – $20m 17. Will Smith $20.5m 16. Chris Pratt $26m 15. Leonardo Dicaprio $27m 14. Salman Khan – $28.5 13. Mark Wahlberg $30m 12. Adam Sandler $30m 11. Brad Pitt – $31.5m 10. Akshay Khumar $31.5m 9. Robert Downey Jr – $33m 8. Shah Rukh Khan – $33m 7. Vin Diesel – $35m 6. Ben Affleck – $43m 5. Johnny Deep – $48m 4. Tom Cruise – $53m 3. Matt Damon – $55m 2. Jackie Chan – $61m 1. Dwayne ‘The Rock’ Johnson $64m
Jarida linalofatilia maisha ya watu maarufu na mali zao “Forbes” limetoa list ya watu matajiri zaidi duniani, na wakati huu kuna mabadiliko makubwa ya watu waliofanikiwa kuingia kwenye Top 10. Bilionea Bill Gates ameendelea kushika nafasi ya kwanza ikiwa ni mara ya 18 kati ya 23 zilizowahi kutajwa.
Kijana mfanyabiashara wa mitandao Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa mitandao maarufu ya kijamii kama Facebook, Whatsapp na Instagram amepanda mpaka nafasi ya 5 mwaka huu.
Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy’ Chande amefariki Dunia. Sir Andy Chande alikuwa mwanachama wa Freemason kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge. Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7, 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora,Tanzania.
Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8 wilayani Kibiti mkoani Pwani jana usiku.
Akizungumza na wanahabari leo, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya majambazi hao.
Amesema baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi, ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao.
Akielezea tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9 waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8 kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi.
Amewataja askari waliuawa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub, ambapo pia walipora bunduki 7 zikiwemo SMG 4.
Kufuatia tukio hilo, Kamishna Marijani ametangaza vita na waharifu wote katika maeneo hayo, ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaanza oparesheni maalum katika mkoa wa Pwani, kuhakikisha vinawasaka na kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua.
Polisi anayedaiwa kumuua mwenzake asakwa kwa dau
“Mpaka sasa jeshi limekwisha poteza skari zaidi ya 10, inatosha…. Tunakwenda kwenye oparesheni maalum, hatutakuwa na mzaha, tutawasaka popote walipo na kuwashughulikia kikamilifu, ,,, watajua tofauti ya moto na maji… mpaka jana idadi ilikuwa ni 8 kwa nne, lakini nawahakikishia kuwa ndani ya wiki moja idadi hiyo itakuwa imebadilika, na tutakuwa na hesabu tofati” amesema Marijani
Kuhusu hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi
Katika hatua nyingine, jeshi hilo limepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki katika maeneo yote ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji zaidi ya saa 12:00 jioni. Amesema usafiri wa boda boda utaruhusiwa kati ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni